1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABIDJAN : Wanajeshi wa Ufaransa watakiwa kuondoka

23 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CD9x

Chama cha Rais Laurent Gbagbo wa Ivory Coast hapo jana kimedai kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa na kuvunjwa kwa timu ya kimataifa yenye kujaribu kukomesha mzozo wa kisiasa nchini humo.

Kiongozi wa chama hicho cha FPI Pascal Affi N’Guessan amewaambia waandishi wa habari kwamba chama hicho kina wasi wasi mkubwa juu ya kugawika kwa nchi hiyo ambako kunaendelea licha ya ridhaa zote za kisiasa zilizotolewa na kiongozi wa nchi Laurent Gbagbo.

Amesema chama cha FPI kinatowa wito wa kuvunjwa kwa timu hiyo ya kimataifa yenye kujumuisha Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya na kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa.

Wito huo unakuja siku chache baada ya Gbagbo kusema kwamba vikosi vya Ufaransa viko huru kuondoka nchini humo na kususia mkutano wa ngazi ya juu kuhusu Ivory Coast wakati wa kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York.