1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMyanmar

29 wauawa katika shambulizi la kambi ya wakimbizi Myanmar

10 Oktoba 2023

Watu 29 wameuliwa na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika shambulizi la jeshi katika kambi ya wakimbizi kaskazini mwa Myanmar.

https://p.dw.com/p/4XMGg
Jeshi la kijeshi la Myanmar limeshutumiwa kwa kutekeleza mashambulizi mengi ya umwagaji damu kwenye maeneo ya raia mnamo wakati likipambana kuzima upinzani dhidi ya mapinduzi yake ya 2021.
Jeshi la kijeshi la Myanmar limeshutumiwa kwa kutekeleza mashambulizi mengi ya umwagaji damu kwenye maeneo ya raia mnamo wakati likipambana kuzima upinzani dhidi ya mapinduzi yake ya 2021.Picha: Khin Maung Win/AP/picture alliance

Hayo ni kwa mujibu wa msemaji wa kundi la waasi wa kikabila wa Jeshi huru la Kachin, linalodhibiti eneo hilo, kanali Naw Bu wakati alipozungmza na shirika la habari la Ufaransa AFP.

Kanali Bu amesema wamepata miili 29 ikiwemo ya watoto na wazee na jumla ya watu 56 walijeruhiwa.

Pia amesema wanachunguza aina ya shambulizi lililoipiga kambi hiyo kwa kuwa hawakusikia mlio wowote wa ndege na wanaangalia kama jeshi lilitumia ndege isiyoendeshwa na rubani kuishambulia kambi hiyo iliyo karibu na mji wa Laiza katika mpaka na China.