Korea Kusini imesema leo katika taarifa yake kwamba sehemu muhimu za mfumo wa ulinzi wa kukinga makombora wa Marekani tayari zimeshawekwa nchini humo, ikiwa ni siku moja baada ya hasimu wake Korea Kaskazini kuonyesha nguvu zake za kijeshi// Marekani imelihimiza baraza lililogawanyika la usalama la Umoja wa Mataifa kuunga mkono marufuku ya uuzaji silaha na vikwazo dhidi ya Sudan Kusini.