Mshauri wa Ikulu ya Marekani, Jared Kushner, amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Israel na Palestina, katika juhudi zinazofanywa na nchi hiyo kuyafufua mazungumzo ya amani ya Mashariki ya Kati, ambayo yamekwama// Qatar imeamuru kufungwa kwa ubalozi wa Chad nchini mwake na kuwapatia masaa 72 wanadiplomasia wake kuondoka, na kuituhumu nchi hiyo kwa kujiunga "na kampeni ya usaliti".