1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rekodi zaonyesha 2024 ulikuwa mwaka wa joto zaidi duniani

10 Januari 2025

Rekodi zinaonesha mwaka uliopita wa 2024 ulikuwa mwaka wa kwanza kamili duniani kuwa na ongezeko la joto lililozidi kiwango kilichowekwa chini ya Mkataba wa kimataifa wa Paris kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa.

https://p.dw.com/p/4p0v1
Indien | Prayagraj | Hitzewelle
Wanawake hutuliza kiu chao kwa maji ya bomba wakati wa joto kali huko Prayagraj India Juni 10, 2024.Picha: Anil Shakya/AFP via Getty Images

Ingawa hata hivyo wanasayansi wanasema bado ulimwengu haujachelewa katika kuchukua hatua ya kuidhibiti hali hiyo.

Taasisi  ya Umoja wa Ulaya ya Huduma ya Mabadiliko ya Tabia Nchiya Copernicus (C3S) imethibitisha katika ripoti yake ya hivi karibuni kwamba mwaka 2024 ndio uliokuwa na joto zaidi kuwahi kurekodiwa Utafiti unaonyesha ongezeko la nyuzi joto 1.6 zaidi ya nyakati za kabla ya zama za kiviwanda, ukielezwa wakati wa miaka ya kati ya 1850 na 1900. Lakini awali mwaka wa joto kali zaidi ulikuwa 2023.

Ulimwengu sasa unaelekea ukingoni mwa kuvuka kiwango cha nyuzi joto 1.5

Katika mkutano wa kimataifa wa mazingira wa Paris mwaka 2015, viongozi 196 wa dunia walikubaliana kupunguza ongezeko la joto duniani lisiwe zaidi ya nyuzi joto 2, na kufuatilia juhudi za kuweka viwango vya joto chini ya nyuzi joto 1.5. Samantha Burgess, ambane ni naibu mkurugenzi wa taasisi C3S aliiambia DW kwamba ulimwengu sasa "unaelekea ukingoni mwa kuvuka kiwango cha nyuzi joto 1.5."

USA Santa Clarita | USA leidet unter extremer Hitzewelle
Helikopta ikidondosha maji mahali penye moto kwenye Moto wa Poppy Julai 10, 2024 huko Santa Clarita, Kaunti ya Los Angeles.Picha: ROBYN BECK/AFP/Getty Images

Aliongeza kuwa ingawa wastani wa miaka miwili iliyopita tayari ulikuwa umevuka kizingiti, haimaanishi kuwa Makubaliano ya Paris yalivunjwa, kwani makubaliano hayo yanategemea wastani uliohesabiwa kwa miongo kadhaa na sikwa mwaka mmoja mmoja. Lakini "inaonyesha mwelekeo tulio nao," huku akionya juu ya athari zake.

Dunia inaashiria kushindwa kudhibiti athari za kimazingira

Dokta Kanizio Freddy Manyika  ni mkurugenzi msaidizi wa masuala wa mabadilio ya tabia nchi na tathimi ya athari zake kwa mazingira katika ya makamo wa rais wa Tanzania. anatoa tafsi ya rekodi hizo."Maana yake ni kwamba,  kama joto la dunia linazidi kuongezeka kuliko miaka yote, eeh tangu kuumbuwa kwa dunia hii, maana yake ni kwamba jitihada ambazo zinafanyika hivi sasa katika kudhibiti gesi joto kutokana na shughuli zinazofanywa na binaadamu hazitoshelezi. Ndio maana gesi joto zimeongezeka, matokeo yake hata joto la dunia ambalo linaleta athari za mabadiliko ya tabia nchi na lenyewe limeongezeka." Alisema Dokta Manyika.

Hadi wakati huu, wastani wa halijoto duniani  kama ilivyopimwa kwa miongo kadhaa imefikia nyuzi 1.3, ongezeko ambalo tayari limesababisha matokeo mabaya.

Mwaka 2024 na athari za matukio yake ya kimazingira

Mwaka 2024 moto wa nyika uliteketeza sehemu za Ardhioevu ya Pantanal nchini Brazil na kuathiri nchi kadhaa katika eneo jirani, huku sehemu za Sudan, Falme za Kiarabu na Uhispania zikikumbwa na mafuriko makubwa. Mawimbi ya joto yalipiga Ulaya na Afrika Magharibi na dhoruba za kitropiki zilikumba sehemu za Marekani na Ufilipino.

Soma zaidi: Mkutano wa COP29 kufunguliwa Jumatatu, Baku

Wanasayansi wanaofanya kazi kama sehemu ya shirika lilipewa jina la "World Weather Attribution", juhudi ya ambayo inachunguza uhusiano kati ya hali mbaya ya hewa na mabadiliko ya taba nchi, na kubaini kuwa matukio 26 kati ya waliyoyafuatilia mwaka jana yamefanywa kuwa mabaya zaidi au ya kutokea  kutokana na kuongezeka kwa joto.

Chanzo: DW: