Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa litaupigia kura baadae leo usiku mswaada wa azimio linaloiruhusu jumuia ya ushirikiano wa kiuchumi Afrika Magharibi-ECOWAS kutuma wanajeshi Gambia ili kuhakikisha utaratibu wa kukabidhi madaraka unapita salama// Serikali ya Uganda imewakamata zaidi ya wapiganaji 100 wazamani wa kundi la M23 wanaojaribu kurejea nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.