Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May leo ametangaza kuitisha uchaguzi na mapema ifikapo Juni 8// Chama kikuu cha upinzani nchini Uturuki kimetuma maombi ya kutaka kura ya maoni ya mageuzi ya katiba ibatilishwe// Serikali ya Tanzania imekuwa ikifanya juhudi za kuimarisha usalama katika wilaya za mkoa wa Pwani za Rufiji na Kibiti, ambapo mauaji yamekuwa yakifanyika.