Mkutano wa siku mbili wa kilele kati ya China na Afrika umemalizika jana mjini Beijing, baada ya majadiliano marefu ya marais na viongozi wa serikali huku Rais wa Senegal Macky Sall akiteuliwa kuwa mwenyekiti mwenza wa ushirikiano wa Afrika na China kwa kipindi cha miaka mitatu akichukua nafasi ya Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa.