1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Lavrov atofautiana na Marekani juu ya mpango wa amani

23 Januari 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi ametofautiana na Marekani na Ukraine katika mkutano wa Umoja wa Mataifa ambapo Moscow imeondoa uwezekano wa kuunga mkono mpango wa amani unaopendekezwa na Ukraine na mataifa ya Magharibi.

https://p.dw.com/p/4bZSl
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergey Lavrov
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergey LavrovPicha: Russian Foreign Ministry Press/dpa/picture alliance

Sergey Lavrov ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa, Urusi iko tayari kujadili mpango wa amani lakini amedai kuwa, mpango unaopendekezwa na Ukraine na mataifa ya Magharibi unatumika tu "kama mbinu ya kuendelea na vita hivyo na kwa Ukraine kuendelea kupokea ufadhili kutoka kwa walipa kodi wa Magharibi."

Mwanadiplomasia huyo wa Urusi amedai kuwa askari wa Ukraine "wameshindwa kabisa" katika uwanja wa mapambano na kwamba hawana uwezo wa kuishinda au hata kuidhoofisha Urusi.

Hata hivyo, naibu balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Robert Wood amepuzilia mbali madai ya Lavrov na kuyataja kama "upotoshaji."

Wood ameeleza kuwa, Urusi ndio iliyoivamia Ukraine na kuanzisha vita hivyo.