1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Urusi kujieleza Umoja wa Mataifa juu ya watoto wa Ukraine

Lilian Mtono
22 Januari 2024

Moscow italazimika kujieleza mbele Umoja wa Mataifa hii leo juu ya kile kilichotokea kwa maelfu ya watoto wa Ukraine wanaoaminiwa kwamba walipelekwa kinguvu nchini Urusi tangu ilipolivamia Ukraine Februari 2022.

https://p.dw.com/p/4bWsP
Ujerumani | Vita vya Ukraine | Urusi
Watoto wakiwa wamevaa bendera ya Ukraine.Picha: Hannibal Hanschke/AP Photo/picture alliance

Kamati ya Haki za Watoto ya Umoja wa Mataifa inayojumuisha wataalamu huru 18 itachunguza rekodi ya Urusi kwa siku mbili, kama sehemu ya ukaguzi wake wa kawaida.

Kwenye orodha ambayo tayari ilitumwa Moscow katika nusu ya kwanza ya mwaka 2023, wataalamu hao wanataka kujua idadi ya watoto waliopelekwa Urusi ama maeneo ya Ukraine yanayokaliwa na Urusi na hatua zilizochukuliwa na Moscow za kulinda haki za watoto kama hao.

Kyiv inasema karibu watoto 20,000 walichukuliwa kinguvu, huku Moscow ikisema inataka kuwalinda dhidi ya mapigano.