1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Robert Fico asema Ukraine inadhibitiwa na Marekani

Amina Mjahid
21 Januari 2024

Waziri mkuu wa Slovakia Robert Fico amesema Ukraine ambayo ni jirani yake sio nchi huru na kwamba inadhibitiwa na Marekani.

https://p.dw.com/p/4bVd0
Slovakia |
Waziri mkuu wa Slovakia Robert Fico Picha: Aureliusz M. Pędziwol/DW

Mwanasiasa huyo mwenye siasa za kizalendo ambaye anapinga msaada wa kijeshi kupelekwa Ukraine na ambaye pia haungi mkono vikwazo dhidi ya Urusi amesisitiza msimamo wake wa kupinga juhudi za Ukraine kujiunga na Jumuiya ya kuhami ya NATO. 

Hungary na Slovakia zapinga msaada wa kifedha kutolewa Ukraine

Waziri mkuu huyo wa Slovakia anatarajiwa kukutana na mwenzake wa Ukraine Denys Shmyhal siku ya Jumatano wiki Ijayo katika mji wa Uzhhorod, Magharibi mwa Ukraine, unaopakana na Slovakia.

Slovakia ni nchi mwanachama wa Jumuiya ya NATO na Umoja wa Ulaya.