1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kimbunga Gamane chaua watu 11 Madagascar

28 Machi 2024

Maafisa nchini Madagascar wamesema watu 11 wamekufa baada ya kimbuga Gamane kuipiga nchi hiyo. Kimbunga hicho Gamane kimefanya uharibifu mkubwa kwenye wa miundombinu na makazi ya watu

https://p.dw.com/p/4eEWS
Bahari ya hindi
Kimbunga Gamane kilichoipiga Madagasca kinatarajiwa kumalizika alasiri ya siku ya ijumaa Picha: AP/picture alliance

    
Maafisa nchini Madagascar wamesema watu 11 wamekufa baada ya kimbuga Gamane kuipiga nchi hiyo. Kimbunga hicho kilitarajiwa kuwa na kasi ya kawaida lakini baadae kilibadili mwelekeo na kutua upande wa kaskazini mwa nchi hiyo ambayo imekuwa ikikabiliwa na majanga ya namna hiyo kwa muda mrefu.

Soma zaidi. Watu 11 wafa kwa kimbunga nchini Madagascar

Kwa mujibu wa ofisi ya kitaifa ya kupambana na majanga nchini Madagascar, zaidi ya watu 7,000 wameathirika na kimbunga Gamane, picha na video mbalimbali zimeonyesha maji mengi yakiwa yamezingira sehemu kubwa ya makazi ya watu.

Picha za video za droni zimeonyesha pia jinsi watu wanavyopambana kuwaokoa wengine ambao wamekwama kwenye maji.

Ofisi hiyo ya kupambana na majanga nchini humo imesema kwa sasa bado upepo mkali unaendela kuvuma kwa kasi kutokea upande wa kaskazini wa nchi hiyo.

Maji ya bahari yaingia mtaani

Mapema hii leo maji ya baharini yalianza kuingia mtaani na kusababisha uharibifu mkubwa ikwemo kuangusha miti na kusomba makazi ya watu katika maeneo ya karibu na fukwe katika taifa hilo la kisiwa.

Indien Zyklon Michuang Michaung
Kwa mujibu wa wataalamu wa hali ya hewa nin kwamba mwezi Novemba hadi Aprili ni msimu wa dhoruba kaliPicha: R. SATISH BABU/AFP/Getty Images

Watu sita wamekufa kwa maji na wengine watano wakipoteza maisha kwa kuporomoka kwa nyumba na miti iliyoanguka, mamlaka ya udhibiti imesema.

Kimbunga hicho cha Gamane kimezunguka kisiwa hicho kikiwa na kasi ya wastani ya upepo wa kilomita 150 kwa saa na mvua kubwa zikiendelea kunyesha,katika maeneo mengine upepo unatajwa kuwa na zaidi ya kilomita 210 kwa saa.

Soma zaidi. Mexico: Watu 48 wafariki dunia kufuatia kimbunga Otis

Mamlaka ya udhibiti wa maafa imearifu kuwa mamia ya nyumba, barabara na madaraja vimefurika maji au kuharibiwa hasa katika maeneo ya kaskazini mwa Madagasca. 

Mpaka sasa kiwango kamili cha uharibifu bado hakijafahamika, kwa sababu vijiji vingi ndani vilivyopo ndani ya eneo hilo vimejitenga mbali na huduma za msingi na kufanya shughuli ya uokozi na kuwafikia kuwa ngumu zaidi.

Novemba hadi April ni miezi ya dhoruba

Kwa mujibu wa wataalam wa hali ya hewa, Kimbuga Gamane kimetajwa kama dhoruba ya kitropiki na kinatarajiwa kutulia kisiwani humo siku ya Ijumaa alasiri.

Gamane
Kimbunga Game kimepelekea maji ya Bahari ya Hindi yameingia kwenye mitaa ya Madagasca na kufanya uharibifu Picha: Romeu da Silva/DW

Soma zaidi. Watu nusu milioni Crimea hawana huduma ya umeme

Msimu wa vimbunga kusini-magharibi mwa Bahari ya Hindi kwa kawaida hutokea kuanzia mwezi Novemba hadi Aprili na dhoruba kali hushuhudiwa kwa wingi kila mwaka.

Taifa hilo la kisiwa lenye wakazi milioni 30 na mabalo lipo kwenye bahari ya Hindi limekuwa likiathiriwa na hali mbaya ya hewa ya mara kwa mara.

Mfano, Mwaka uliopita Kimbunga Freddy kiliipiga nchi hiyo na kuharibu sehemu kubwa ya nchi hiyo na mataifa mengine ikiwemo Msumbiji na Malawi ambapo zaidi ya watu 500 walipoteza maisha.