1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaMauritius

Mauritius yatoa tahadhari ya kimbunga Belal

16 Januari 2024

Mauritius ipo katika tahadhari ya hali ya juu kufuatia kimbunga Belal kilichoambatana na upepo mkali na mvua. Kimbunga hicho kimesababisha uharibifu katika kisiwa hicho huku serikali ikiamuru wakaazi wote kusalia ndani.

https://p.dw.com/p/4bJHS
Indien | Überschwemmung in Chennai | Sturm Mischaung in  Südindien
Kimbunga Belal kimesababisha maelfu ya watu kukosa umemePicha: R. Satish Babu/AFP

Kimbunga Belal kimesababisha maelfu ya watu kukosa umeme na magari kadhaa kusombwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa.

Polisi wameripoti kuupata mwili wa mwendesha pikipiki katika barabara kuu iliyofurika.

Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mauritius ulikuwa umefungwa jana Jumatatu (15.01.2024) huku shirika la ndege la nchi hiyo likitangaza kufuta safari kadhaa za ndege zilizopangwa leo Jumanne.

Februari mwaka jana, Mauritius ilikumbwa na mvua kubwa na upepo mkali kutokana na kimbunga Freddy, ambacho kilisababisha wimbi la vifo na uharibifu katika nchi za kusini mashariki mwa Afrika zikiwemo Malawi, Msumbiji na Madagascar.