1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaLibya

Watu 10,000 haijulikani waliko baada ya mafuriko Libya

13 Septemba 2023

Vifo kutokana na mafuriko nchini Libya huenda vikaongezeka. Hadi sasa jumla ya watu 2,300 ndio wameripotiwa kufariki dunia, lakini mamlaka nchini humo zimebaini kuwa takriban watu 10,000 hadi sasa haijulikani waliko.

https://p.dw.com/p/4WGUr
Überschwemmungen in Libyen
Picha: Jamal Alkomaty/AP Photo/picture alliance

Mafuriko hayo yamesababisha uharibifu mkubwa wa majumba, magari na miundombinu muhimu kama barabara na madaraja. Zaidi ya watu 40,000 wamelazimika kuyahama makazi yao. Uharibifu mkubwa umeshuhudiwa katika mji wa mashariki wa Derna.

Soma pia: Vifo kutokana na mafuriko vyafikia 2,300 Libya

Mataifa kadhaa kama Ujerumani, Ufaransa na Italia yameahidi kutuma vikosi vya waokoaji pamoja na misaada. Serikali yenye makao yake mjini Tripoli imetuma msaada wa tani 14 wa vifaa vya matibabu na wahudumu wa afya na kwamba imetenga dola milioni 412 kwa ajili ya kuijenga upya Derna na miji mingine ya Mashariki mwa Libya.