1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
BiasharaChina

Rais Xi Jinping atoa wito wa ushirikiano na Marekani

Lilian Mtono
27 Machi 2024

Rais wa China Xi Jinping ametoa wito wa ushirikiano wa karibu wa kibiashara na Marekani wakati wa mkutano na viongozi wakuu wa kibiashara wa nchi hiyo mjini Beijing.

https://p.dw.com/p/4eBdl
Marekani | Xi Jinping akutana na Joe Biden
Rais wa China Xi Jinping na Rais Joe Biden wa Marekani wakati Xi alipozuru Washington Novemba 15, 2023 Picha: Doug Mills/AP Press/picture alliance

Mkutano huo unafanyika wakati mahusiano kati ya mataifa hayo mawili yakiaanza kuimarika baada ya kudorora kwa miaka kadhaa.

Xi amesisitiza leo kuhusu mahusiano hayo ya kiuchumi yenye manufaa kwa mataifa hayo mawili yenye uchumi mkubwa zaidi duniani, licha ya ushuru mkubwa unaotozwa na Marekani kwenye manunuzi ya bidhaa za China.

Xi amenukuliwa na shirika la habari la nchi hiyo Xinhua akisema kuwa mahusiano ya China na Marekani ni moja ya mahusiano muhimu zaidi kati ya mataifa mawili kote duniani na yanayotoa mwelekeo wa siku za baadaye.

Washiriki katika mkutano huo ni pamoja na Stephen A. Schwarzman, mkuu wa kampuni ya uwekezaji ya Blackstone.