1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiSudan

WFP: Sudan kuwa "janga kubwa zaidi la njaa duniani"

Tatu Karema
6 Machi 2024

Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa WFP limeonya leo kuwa vita vya karibu miezi 11 nchini Sudan kati ya majenerali hasimu vinahatarisha kutokea janga kubwa la njaa duniani.

https://p.dw.com/p/4dDX1
Wakimbizi wa Sudan Kusini wakipanga foleni kupokea mgao wa chakula katika kambi ya Bidi Bidi
Wakimbizi wa Sudan Kusini wakipanga foleni kupokea mgao wa chakula katika kambi ya Bidi BidiPicha: Alda Tsang/ZUMA Press/IMAGO

Mkurugenzi Mtendaji wa WFP Cindy McCain amesema kwasasa, maisha ya mamilioni, amani na utulivu wa eneo zima ziko hatarini.

McCain ameongeza kuwa miaka 20 iliyopita, eneo la Darfur ndilo lililokuwa na mzozo mkubwa zaidi wa njaa duniani na dunia ilijotolea kulisaidia akimaanisha eneo kubwa la Magharibi mwa Sudan, lakini sasa ni watu wa Sudan waliosahaulika.

Soma pia: Umoja wa Mataifa waituhumu RSF kwa uhalifu wa kivita Darfur 

Mkuu huyo wa WFP amesema kwasasa, shirika hilo haliwezi kufikia asilimia 90 ya wale wanaokabiliwa na viwango vya dharura vya njaa na kwamba ni asilimia tano tu ya idadi ya watu wa Sudan wanaoweza kupata mlo mmoja kwa siku.