1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Sudan lazuwia misaada kuelekea Darfur

Tatu Karema
26 Februari 2024

Serikali inayoongozwa na jeshi nchini Sudan imezuia misaada inayopelekwa katika la eneo la Darfur Magharibi, hatua iliyozusha shutuma kali kutoka kwa wafanyakazi wa misaada na Marekani.

https://p.dw.com/p/4cuBp
Magunia ya ngano kwenye soko kuu la Gedarf, mashariki mwa Sudan.
Magunia ya ngano kwenye soko kuu la Gedarf, mashariki mwa Sudan.Picha: Ebrahim Hamid/AFP

Umoja wa Mataifa umelazimika kupunguza shughuli zake za kuvuusha msaada huo kutoka Chad kuelekea Darfur.

Wiki iliyopita, Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Eddie Rowe, aliwaambia waandishi habari kwamba mamlaka nchini Chad imezuia operesheni hiyo ya kuvuusha misaada.

Siku ya Ijumaa, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Marekani, Matthew Miller, alisema nchi yake ina wasiwasi mkubwa kuhusu hatua hiyo ya jeshi ya kuzuwia misaada kutoka nje.

Hata hivyo, wizara ya mambo ya nje ya Sudan imeelezea kughadhabishwa na madai hayo iliyoyaita ya uongo kutoka Marekani.

Wizara hiyo imesema mpaka kati ya Sudan na Chad ndio njia kuu inayotumika kupitisha silaha na vifaa vinavyotumika kufanya uasi dhidi ya raia wa Sudan.