1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi, Ukraine zatupiana lawama kuanguka ndege ya wafungwa

Bruce Amani
25 Januari 2024

Urusi na Ukraine zimetupiana lawama kuhusu kuanguka kwa ndege ya kijeshi ambayo Moscow ilisema ilikuwa imewabeba wafungwa wa kivita wa Ukraine na ilidunguliwa na vikosi vya Kyiv.

https://p.dw.com/p/4bg3K
Urusi, Ukarine, Belgorod
Mabaki ya ndege ya kijeshi ya Urus iliyoanguka na kuuwa watu wote 74 waliokuwamo, miongoni wafungwa 65 wa kivita wa Ukraine, kwa mujibu wa Urusi.Picha: TASS/dpa/picture alliance

Ijapokuwa wachunguzi wamedaiwa kupata visanduku vya kuhifadhi taarifa za safari siku moja baada ya kuanguka kwa ndege hiyo jana, kuna matumaini madogo ya kufahamu kilichosababisha tukio hilo huku kila upande ukitupiana lawama ijapokuwa hakuna aliyetoa ushahidi wa kuthibitisha hilo.

Ndege hiyo ilianguka katika eneo la Belgorod nchini Urusi na maafisa wakasema watu wote 74 waliokuwemo, ikiwa ni pamoja na wafungwa 65 wa kivita, waliuawa.

Soma zaidi: Ukraine yataka uchunguzi wa kimataifa katika ajali ya ndege ya Urusi

Urusi kupitia msemaji wa Ikulu ya Kremlin, Dmitry Peskov, inadai kuwa Kyiv iliidungua ndege hiyo na makombora mwili na kusema wafungwa hao wa kivita walikuwa njiani kwenda kubadilishwa na wa Urusi.

Ukraine ilijibu kwa kuituhumu Urusi kwa kusambaza propaganda.

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine ametoa wito wa kufanywa uchunguzi wa kimataifa kuhusu tukio hilo