1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiongozi wa kijeshi wa Chad atangaza kuwania urais

Iddi Ssessanga
2 Machi 2024

Mkuu wa utawala wa kijeshi nchini Chad Mahamat Idriss Deby Itno amesema leo kuwa atawania uchaguzi wa rais wa Mei 6, siku tatu tu baada ya mpinzani wake mkuu kuuawa katika mazingira ya kutatanisha.

https://p.dw.com/p/4d6dT
Mkuu wa utawala wa kijeshi nchini Chad Mahamat Idriss Deby Itno
Mkuu wa utawala wa kijeshi nchini Chad Mahamat Idriss Deby ItnoPicha: Denis Sassou Gueipeur/AFP

Deby Itno alichukuwa madaraka mwaka 2021 baada ya baba yake, kiongozi mkongwe Idriss Deby Itno, kufariki wakati akipambana na waasi.

Kiongozi huyo alietawala kwa mkono wa chuma alikuwa ameiongoza nchi hiyo kwa zaidi ya miongo mitatu. Deby Itno alitangazwa kuwa rais wa mpito na uongozi wa kijeshi na aliahidi kurejesha utawala wa kiraia na uchaguzi katika kipindi cha miezi 18.

Lakini aliongeza kipindi cha mpito kwa miaka miwili. Tarehe ya uchaguzi ilitangazwa siku ya Jumanne, chini ya miezi miwili kabla ya kura.

Soma pia:Kiongozi wa upinzani Chad auawa katika shambulizi la kijeshi

Deby Itno mwenye umri wa miaka 39 ana uhakika wa kushinda kutokana mpinzani wake mkuu Yaya Dillo Djeru kuuawa siku ya Jumatano, na upinzani kukandamizwa.