1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Nancy Faeser alaani shambulio la kisu Solingen

24 Agosti 2024

Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Nancy Faeser amesema kuwa taifa hilo limeshtushwa na shambulio la kisu lililosababisha vifo vya watu watatu katika mji wa Solingen.

https://p.dw.com/p/4jsRF
Ujerumani I Nancy Faeser
Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Nancy FaeserPicha: Frederic Kern/Geisler-Fotopress/picture alliance


Feaser aliyetoa kauli yake kupitia jukwaa la X amelitaja shambulio hilo kuwa ni la kikatili na kuongeza kuwa, polisi wanafanya kila wawezalo ili kumkamata aliyehusika na shambulio hilo. 

Tukio hilo la Ijumaa usiku lilitokea baada ya mtu mmoja kuvamia tamasha la  kusherehekea miaka 650 ya kuanzishwa kwa mji huo ulio magharibi mwa Ujerumani. Takribani watu wanane wamejeruhiwa katika mkasa huo huku watano kati yao wakiripotiwa kuwa na majeraha makubwa.

Taarifa ya polisi imesema kuwa kwa sasa msako mkali unaendelea ili kumkamata mhusika wakati wakiendelea kuwahoji waathiriwa na mashuhuda wa tukio hilo.