1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroLebanon

Waziri Mkuu wa Lebanon alaani "mpango wa uharibifu"

23 Septemba 2024

Waziri Mkuu wa Lebanon Najib Mikati amelaani kile alichokiita "mpango wa uharibifu", huku kukiripotiwa hivi leo mashambulizi makali ya Israel mashariki na kusini mwa Lebanon.

https://p.dw.com/p/4kzAT
Lebanon Najib Mikati
Waziri Mkuu wa Lebanon Najib Mikati amelaani mashambulizi yaliyofanywa na Israel nchini mwakePicha: Mohamed Azakir/REUTERS

Mikati amelihimiza Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na nchi zenye ushawishi kuuzuia uchokozi  huo wa Israel.

Waziri wa Habari wa Lebanon Ziad Makary amesema " Uchokozi unaoendelea wa Israel dhidi ya Lebanon, bila shaka ni vita vya maangamizi na mpango wa uharibifu."

Wizara ya afya ya Lebanon imesema mashambulizi ya Israel ya leo Jumatatu yamesababisha vifo vya watu 182, huku wengine zaidi ya 700 wakijeruhiwa ikiwa ni pamoja na watoto, wanawake na madaktari.

Iran imeonya kuhusu uwezekano wa matokeo ya hatari kufuatia mashambulizi hayo.