1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 15 wauwawa katika shambulizi la Israel mjini Gaza

26 Septemba 2024

Waokoaji wa wakala wa ulinzi wa umma katika Ukanda wa Gaza wamesema shambulizi la Israel katika shule iliyogeuzwa kuwa makazi limewaua watu wapatao 15, huku jeshi la Israel likisema limekilenga kituo cha kundi la Hamas.

https://p.dw.com/p/4l7b6
Gaza| Mashariki ya Kati
Israel inaendelea kuvurumisha makombora katika Ukanda wa Gaza Picha: DW/Arte/ZDF

Msemaji wa wakala wa ulinzi Mahmud Bassal amesema kuna mashahidi saba, wakiwemo watoto, na watu wengi wamejeruhiwa kufuatia shambulizi la kombora la Israel lililoilenga shule ya Al-Faluja katika kambi ya Jabalia kaskazini mwa Gaza.

Ulimwengu wataka Mashariki ya Kati isitumbukie vitani

Jeshi limethibitisha limefanya mashambulizi kuwalenga wanamgambo wa Hamas wanaoendesha shughuli zao katika kile walichokiita kuwa ni kituo cha kamandi na udhibiti katika shule hiyo.