wafuasi wa Laurent Nkunda waendelea kuzusha hofu Kongo
30 Agosti 2007Matangazo
Wanamgambo hao wanaomuunga mkono Kiongozi wa waasi Laurent Nkunda waliwavamia na kuwashambulia wanajeshi hao huko mashariki mwa jimbo la Kivu kaskazini.
Takriban wanamgambo 900 waliwavamia wanajeshi wa serikali katika eneo la Rubaya kiasi kilomita 60 kutoka mji wa Goma.