1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikosi vya Pakistan vyawaua wanamgambo wanane

26 Septemba 2024

Maafisa wa usalama wa Pakistan wamewaua wanamgambo wanane katika ngome ya zamani ya Taliban nchini Pakistan katika eneo linalokabiliwa na machafuko la kaskazini magharibi linalopakana na Afghanistan.

https://p.dw.com/p/4l7Yp
Pakistan
Maafisa wa usalama wa Pakistan wamewaua wanamgambo kadhaa katika ngome ya zamani ya TalibanPicha: picture alliance / ZUMAPRESS.com

Hayo ni kwa mujibu wa jeshi la Pakistan. Jeshi hilo limesema katika taarifa kwamba vikosi vyake pia vimechukua silaha na risasi kutoka kwenye maficho ya wapiganaji kufuatia ufyetulianaji mkali wa risasi katika wilaya ya Waziristan Kaskazini, jimbo la Khyber Pakhtunkhwa.

Jeshi halikutoa taarifa kuhusu wanamgambo waliouliwa, ikiwamo washirika wanaohusiana nao.