1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa wapitisha "Mkataba wa Mustakabali"

23 Septemba 2024

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeidhinisha makubaliano ya kuyaleta pamoja mataifa yanayotafautiana sana ulimwenguni kwenye kukabiliana na changamoto za karne ya 21.

https://p.dw.com/p/4kxS4
Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.Picha: John Lamparski/NurPhoto/picture alliance

Changamoto hizo zinaanzia kwenye zile za mabadiliko ya tabianchi na akili mnemba hadi vita vinavyoendelea na ongezeko la ukosefu wa usawa na umasikini. 

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeidhinisha makubaliano ya kuyaleta pamoja mataifa yanayotafautiana sana ulimwenguni kwenye kukabiliana na changamoto ya karne ya 21 kutoka zile za mabadiliko ya tabianchi na akili mnemba hadi vita vinavyoendelea na ongezeko la ukosefu wa usawa na umasikini.

Soma zaidi: Hadhara kuu ya UN yaidhinisha mkataba wa mageuzi ya Umoja wa Mataifa

Makubaliano hayo yenye kurasa 42 kwa jina la "Mkataba kwa ajili ya Mustakabali" yanawataka viongozi wa mataifa 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa kuzigeuza ahadi zao kuwa vitendo vikavyobadili maisha ya zaidi ya watu bilioni nane duniani.

Makubaliano hayo yalipitishwa kwenye ufunguzi wa mkutano wa siku mbili juu ya Mustakabali ulioitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja huo, Antonio Guterres, hapo jana.

Guterres aliwashukuru viongozi kwa kupiga hatua ya kwanza na kufunguwa mlango kuekelea mustakabali mwema kwa ulimwengu.

Hata hivyo, mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa aliwaonya kwamba sasa ni muda wa kuyatekeleza makubaliano hayo.