1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maafisa Saxony,Ujerumani walijitahidi kuzuia al Bakr kujiua

Jane Nyingi
13 Oktoba 2016

Madai ya maafisa wa sheria katika jimbo la Saxony hapa Ujerumani kuwa walifanya kila wawezalo kumzuia mshukiwa wa Ugaidi Jaber al Bakr kujiua wakati akiwa gerezani yamepokelewa kwa mashaka na kukosolewa vikali.

https://p.dw.com/p/2RCUl
Fahndung nach Syrer Dschaber Al-Bakr nach Sprengstoff-Fund in Chemnitz
Picha: picture-alliance/dpa/Polizei Sachsen

Hata mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika leo katika mji mkuu wa jimbo la Saxony wa Dresden haukutoa maelezo ya kutosha kuhusu uchunguzi unaoendelea wa jaribio la al Bakr kushambulia kwa bomu uwanja wa ndege wa Berlin.

Katika mkutano huo wa waandishi wa habari waziri wa sheria jimbo la Saxony Sebastian Gemkow amesema Jaber al-Bakr mwenye umri wa miaka 22 alijinyonga kwa kutumia shati katika gereza alilokuwa akizuiliwa. Gemkow hata hivyo amesema atawajibika kisiasa juu ya mauji hayo ,lakini hatojizulu.Waziri huyo amekosolewa kutokana na jinsi alivyoshughulikia tukio hilo tangu mwanzo hasa baada ya mshukiwa kuwakwepa polisi siku ya Jumamosi walipokuwa wakijiandaa kuvamia ghorofa alilokuwa akiishi Al-Bakr katika mji wa Chemnitz"Tulifanya mazungumzo na mtuhumiwa ili kupata picha sahihi kumhusu, pia maafisa wanaotoa huduma za kisaikolojia katika gereza alilokuwa akizuiliwa walifanya mazungumzo nae na hawakugundua dalili zozote za kutaka kujiua. Hayo yalithibitishwa katika mkutano wa idara." alisema Gemkow

Berlin Anti-Terror-Einsatz Polizei am Flughafen Schönefeld
Polisi wakiyakagua magari uwanja wa ndege wa Berlin-SchönefeldPicha: Getty Images/C. Bilan

Al-Bakr anashukiwa alikuwa akipanga kushambulia kwa bomu uwanja wa ndege wa Berlin.Inadaiwa mshukiwa huyo alikuwa amewaeleza polisi kuwa wakimbizi watatu raia wa Syria waliomtia mbaroni na kisha kumkabidhi kwa polisi walikuwa washirika wake. Hata hivyo mwendesha mashtaka Klaus Freishmann alisema hawako chini ya uchunguzi.Badala yake watu hao watatu wamesifiwa na vyombo vya habari na hata wanasiasa hhapa ujerumani wakitajwa kuwa mashujaa.Mkuu wa gereza alilokuwa akizuiliwa mtuhumiwa, Rolf Jacob amesema hakimu alikuwa tayari amewaarifu al-Bakr yuko katika hatari ya kujitoa uhai baada ya kususia chakula tangu alipotiwa mbaroni. "Baada ya mazungumzo ya kina , mwanasaikolojia aliondoa wasiwasi wowote wa mshukiwa kujiua na kwa hivyo alitoa pendekezo kwa idara husika kuongeza muda wa kumtembelea mshukiwa kwenye seli kutoka dakika 15 hadi 30." alisema Jacob

Wanasiasa hapa ujerumani wameghadhabishwa na kifo hicho .Katika gazeti la Deutschland funk mwanasiasa wa chama cha mazingira Konstantin von Notz alitaja kujitoa uhai al-bakr kuwa kashfa isiyoeleweka,huku mwanasiasa wa chama cha Christain Democrat Wolfgang Bosbach akisema kifo hicho ni janga kwa kuwa angetoa taarifa muhimu ambazo zingesaidia katika uchunguzi.

Mwandishi:Jane Nyingi/DPAE/APE

Mhariri:Yusuf Saumu