Uchaguzi wa rais mpya wa Libanon umeahirishwa
30 Novemba 2007Matangazo
Bunge la Libanon kwa mara nyingine tena limeahirisha uchaguzi wa rais mpya.Rais wa bunge Berri amesema,serikali ya mseto inayoelemea kambi ya magharibi na upinzani unaoiunga mkono Syria zinahitaji muda zaidi kumtafuta mwanasiasa atakaekubaliwa na pande zote mbili.