1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN:Iran yasema itaendelea na urutubishaji wa madini ya Uranium

20 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG5k

Iran imetangaza hii leo kwamba itajibu rasmi tarehe 22 mwezi Agosti juu ya mapendekezo iliyopewa na nchi za magharibi ya kuishawishi kuachana na mpango wake wa Kinuklia.

Lakini wakati huo huo baraza kuu la usalama la Iran limetishia kuzifikiria upya sera za Iran juu ya Nukilia endapo nchi hiyo itawekewa vikwazo.

Kutokana na kile kinachoonekana kama ni jibu la Urussi kwa kile ilichodokeza kwamba serikali ya Moscow itafikiria juu ya vikwazo dhidi ya Iran, Afisa wa ngazi ya juu kwenye baraza hilo la usalama la Iran amesema nchi yake itaendelea na kazi yake ya kurutubisha madini ya Uranium na kulionya baraza la usalama la Umoja wa mataifa dhidi ya kuchagua njia ya kutumia nguvu kuutatua mgogoro huu.