Muhtasari wa taarifa ya habari: Mtoto mwenye umri wa miezi sita ambaye alipigwa na polisi wakati walipovamia eneo la mabanda nchini Kenya amefariki dunia akiwa hospitali. Rais Donald Trump amerejea kuzilaumu pande zote katika vurugu za Charlottesville. Na Colombia imetangaza kumalizika kwa mgogoro na waasi wa FARC.