1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SUMATRA. Misaada ya kibinadamu yaanza kupokelewa Indonesia.

30 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFRz

Misaada ya kibinadamu imeanza kuwasili katika sehemu zilizoathirika na tetemeko la ardhi huko Indonesia.

Tetemeko la ardhi lenye vipimo vya rishta 8.7 liliikumba pwani ya Sumatra nchini Indonesia siku ya jumatatu na kuathiri vibaya visiwa vya Nias na Simeulue.

Kutokana na uharibifu mkubwa wa barabara na mawasiliano kumesabisha kuchelewa kwa misaada, Uwanja wa ndege wa Nias hauwezi kutumika na barabara nyingi zimeharibiwa vibaya.

Wahusika wamehakikisha kuwa zaidi ya watu 330 wameuwawa katika visiwa vyote viwili, yumkini watu zaidi ya 1000 yahofiwa wameuwawa.