1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH:Chama cha Fatah chajipatia ushindi Ukingo wa Magharibi

1 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEVz

Tume ya uchaguzi nchini Palestina leo imetangaza matokea ya mwisho ya uchaguzi wa serikali za mitaa katika ukingo wa magharibi.

Chama cha Fatah kinachoongozwa na rais Mahmoud Abbas kimejisombea viti 51 vya mabaraza ya miji huku kundi la Hamas likijizolea viti 13 pekee.

Viti 104 vya mabazara ya miji vilikuwa vinagombaniwa ukingo wa magaharibi huu ukiwa ni uchaguzi wa kwanza katika kipindi cha miongo mitatu.

Viti vingine 40 vilivyasalia vilisombwa na makundi mengine.