1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

RAMALLAH. Chama cha Fatah chashinda uchaguzi wa serikali za mitaa.

6 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFGE

Chama cha Fatah kikiongozwa na rais Mahmoud Abbas kimeshinda uchaguzi wa serikali za mitaa katika ukingo wa magharibi na mkanda wa Gaza. Afisa wa uchaguzi amesema chama hicho kimejipatia asilimia 59.9 ya kura dhidi ya kundi la Hamas ambalo limejipatia asilimia 33.3 ya kura zote zilizopigwa.

Kura hiyo inaonekana kama mtihani kwa umaarufu wa chama cha Hamas, miezi miwili tu kabla kufanyika uchaguzi wa bunge unaotarajiwa kufanyika mwezi Julai mwaka huu.