OAXACA : Polisi yadhibiti mji wa Oaxaca nchini Mexico
30 Oktoba 2006Matangazo
Polisi wa kutukiza ghasia nchini Mexico wameukalia mji wa kusini wa Oaxaca ambapo waandamanaji wamekuwa wakiaandamana dhidi ya gavana wa jimbo hilo kwa miezi mitano.
Wakisaidiwa na helikopta na magari ya deraya polisi hao walivunjulia mbali vizuizi vilivyowekwa barabarani na waadamanaji na hawakukumbana na upinzani mkubwa.
Machafuko hayo yalianza hapo mwezi wa Mei wakati walimu waliokuwa wakigoma na wafuasi wa sera za mrengo wa shoto walipotwaa eneo la katikati ya mji huo.
Vyombo vya habari vya Mexico vimeripoti kwamba walimu wanaofikia 70,000 ambao walikuwa wakidai mishahara mikubwa zaidi hivi sasa wamekubali kurudi kazini leo hii.