1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Noboa ashinda uchaguzi wa urais Equador

16 Oktoba 2023

Daniel Noboa, mwenye umri wa miaka 35, amemshinda msoshalisti Luisa Gonzalez, mwenye umri wa miaka 45, kwenye kura ya marudio.

https://p.dw.com/p/4XZW0
Ecuador, Olon | Presidentschaftskandidat Daniel Noboa
Picha: Martin Mejia/AP/picture alliance

Baada ya asilimia 93 ya kura kuhesabiwa, Noboa alikuwa mbele kwa asilimia 52 huku Gonzalez akiwa wa pili kwa asilimia 48.

Baraza la uchaguzi nchini humo limesema kulingana na kura zilizokwisha hesabika, matokeo hayo hayawezi yakabadilika.

Gonzalez amekubali kushindwa na amempongeza Noboa kwa ushindi wake. 

Soma zaidi: Ecuador: Daniel Noboa ashinda uchaguzi wa rais

Amesema hayo alipokuwa akizungumza na wafuasi wake mjini Quito.

Wagombea hao wawili walishiriki kura ya marudio baada ya kuchukua nafasi ya kwanza na pili mbele ya wagombea wengine sita katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa Agosti 22.

Masuala makuu ambayo yanawapa wapiga kura changamoto nchini humo ni pamoja na uchumi ambao umetatizika tangu kutokea kwa janga la UVIKO-19, ongezeko la uhalifu ikiwemo mauaji na ghasia za magerezani.