1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Niamey. Waandamanaji wapinga kupanda kwa bei ya vyakula nchini Niger.

9 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFOw

Maelfu ya watu wameingia katika mitaa ya mji mkuu wa Niger leo wakipinga dhidi ya kuongezeka kwa bei ya bidhaa muhimu katika taifa hilo masikini barani Afrika.

Waandamanaji hao walirejea makwao kimya kimya hata hivyo baada ya hotuba mbali mbali, lakini katika mji wa kaskazini wa Agadez, watu zaidi ya kumi na mbili walijeruhiwa baada ya polisi kuwatawanya waandamanaji zaidi ya 1,000 kwa mabomu ya kutoa machozi.

Katika mji mkuu Niamey polisi walibaki kando mbali na waandamanaji hao huku waandamanaji wakibeba mabango na kusema hatutaki serikali ya waongo na walaaniwe wanyonyaji damu za wananchi.