1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Ukuta ni kikwazo dhidi ya amani mashariki ya kati, asisitiza Yasser Arafat-

2 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFvy
Muwakilishi wa mamlaka ya wapalestina kwenye umoja wa mataifa, jana aliisoma barua ya kiongozi wao kwa Jumuia hiyo, ambapo Rais Yasser Arafat anaonya ukuta unaojengwa na Israel baina ya nchi hio na ardhi za wapalestina, ni kikwazo kikubwa kwa amani na utulivu katika eneo la mashariki ya kati.

Bwana Nasser Al Kidoua aliisoma barua hio katika sherehe zinazofanyika kila mwaka, za siku ya kimataifa ya usaidizi kwa wapalestina.

Barua hiyo ya Rais Yasser Arafat kwa umoja wa mataifa, imesomwa mda mfupi baada ya kusainiwa nchini Usuwisi, mkataba wa makubaliano ya amani, baina ya wanasiasa wa upinzani nchini Israel, na viongozi wa kipalestina.

Waziri mkuu wa Israel Ariel Sharon ambae ametupilia mbali azimio la umoja wa mataifa linalomtaka kusitisha ujenzi wa ukuta baina ya nchi yake na ardhi za wapalestina, anapinga vikali pia makubaliano yaliyofikiwa baina ya wanasiasa wa upinzani na viongozi wa kipalestina, yenye lengo la kusitisha uhasama baina ya wayahudi na wapalestina-