1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Niger ukingoni mwa maafa ya kibinadamu.

20 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEsg

Umoja wa mataifa umesema kuwa nchi ya Niger iliyoko magharibi mwa bara la Afrika imo ukingoni mwa kutumbukia katika maafa ya kibinadamu.

Maafisa wa umoja wa mataifa pamoja na madaktari wa kimataifa nchini humo wanasema watoto wanakufa kutokana na njaa kwa sababu dunia imepuuzia miito yao ya kupatiwa misaada ya chakula.

Mazao nchini Niger yameharibika kutokana na baa la nzige pamoja na ukame.

Mkuu wa masuala ya kibinadamu katika umoja wa mataifa amesema kuwa watu milioni 2.5 nchini Niger wako katika hali mbaya ya mahitaji ya chakula ikiwa ni pamoja na watoto 800,000 ambao wanakabiliwa na utapia mlo.