1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAfrika

Nchi za Mashariki mwa Afrika zaongoza kwa maambukizi HIV

22 Julai 2024

Umoja wa Mataifa umesema leo,kwamba maamuzi ya kisiasa yanayochukuliwa mwaka huu yataamuwa ikiwa lengo la kuutokomeza kabisa ugonjwa wa Ukimwi kama kitisho kwa afya ya umma, kufikia mwaka 2030 litafikiwa au la.

https://p.dw.com/p/4ibfA
Mkutano wa Kimataifa wa Ukimwi
Mkutano wa Kimataifa wa UkimwiPicha: Sabine Dobel/dpa/picture alliance

 Takwimu kutoka mwaka 2023 zinaonesha maambukizi mapya ya virusi vinavyosababisha ugonjwa huo, na vifo vimepunguwa na kumeshuhudiwa hali iliyoimarika ya upatikanaji wa tiba kwa wagonjwa. 

Hata hivyo shirika la kupambana na Ukimwi la Umoja wa Mataifa, UNAIDS limetahadharisha kwamba hatua zilizopigwa bado ni dhaifu. Mkuu wa shirika hilo Winnie Byanyima akizungumza mjini Munich kunakofanyika mkutano wa kimataifa kuhusu kupambana na Ukimwi, amesema bado ulimwengu umebakia nyuma kuelekea malengo ya 2030. 

Soma pia:WHO yathibitisha kisa cha maambukizi ya mafua ya ndege kwa binadamu India

Mataifa ya Mashariki na Kusini mwa Afrika yametajwa kuendelea  kuwa maeneo yenye maakumbukizi zaidi. Watu milioni 20.8 wanaishi na HIV na 450,000 waliambukizwa mwaka jana.

Lakini pia kanda hiyo inatajwa kuwa moja ya maeneo yaliyopata mafanikio makubwa ya kupunguza maambukizi mapya kwa asilimia 59 tangu mwaka 2010.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW