Ikiwa imebakia miezi minne kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini Kenya, muungano wa upinzani National Super Alliance, NASA bado haujatangaza jina la mgombea wake katika kinyang'anyiro cha urais. Herman Manyora ni mchambuzi wa masuala ya kisiasa na hapa anaeleza kwanini NASA haijamtangaza mgombea wao hadi sasa.