1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanadiplomasia mkuu wa Iran akamilisha ziara yake UAE

22 Juni 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Iran amehitimisha ziara yake ya siku tatu kwenye mataifa jirani ya Ghuba ya Arabuni, kwa kuzuru Umoja wa Falme za Kiarabu ambako alikutana na Rais Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan.

https://p.dw.com/p/4SxIv
VAE Abu Dhabi | Herrscher Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan
Picha: Jon Gambrell/AP/picture alliance

Ziara ya Hossen Amir-Abdollahia katika Umoja wa Falme za Kiarabu, inafanyika baada ya kuzuru Qatar, Kuwait na Oman, ikiwa ni hatua ya karibuni zaidi katika msururu wa hatua za kidiplomasia za Tehran inayotaka kupunguza kutengwa, kuboresha uchumi wake na kuimarisha miradi yake.

Mapema leo, viongozi hao walijadiliana kuhusu mahusiano baina ya mataifa yao na namna ya kuimarisha uhsirikiano, hii ikiwa ni kulingana na shirika la habari la WAM la Umoja wa Falme za Kiarabu, wakati mataifa ya Ghuba yakiangazia kupunguza mivutano na Iran iliyochochewa katika miaka ya karibuni na mizozo ya Yemen na Syria.

Kwenye ziara hiyo, Iran ilisaini makubaliano na Umoja wa Falme za Kiarabu ya kutanua huduma usafiri wa anga na kuongeza fursa za biashara na utalii,