1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UhalifuUjerumani

Msyria akamatwa baada ya shambulizi mjini Essen

Hawa Bihoga
29 Septemba 2024

Mshukiwa raia wa Syria amekamatwa baada ya moto kuzuka kwenye majengo mawili ya makaazi na basi dogo kuparamia maduka katika mji wa magharibi mwa Ujerumani wa Essen.

https://p.dw.com/p/4lD0d
Polisi kwenye eneo la mkasa mjini Essen
Polisi kwenye eneo la mkasa mjini Essen.Picha: Markus Gayk/picture alliance/dpa

Polisi katika mji huo wa Essen imesema katika taarifa kuwa watu zaidi ya 30 wamejeruhiwa katika moto uliozuka Jumamosi usiku, wakiwemo watoto wanane waliojeruhiwa vibaya.

Muda mfupi baadaye, basi dogo liligonga maduka mawili ya karibu, na kusababisha uharibifu lakini hakukuwa na majeruhi, imeongeza polisi na kusema mwanaume raia wa Syria mwenye umri wa miaka 41 alikamatwa kwenye eneo la tukio.

Uchunguzi wa awali umebainisha kuwa mshukiwa huyo alifanya kitendo hicho baada ya kuachwa na mke wake, huku polisi ikisema alitoka akiwa amejihami na visu na vichochezi vya moto akikusudia kulenga nyumba na maduka mjini Essen, yanayohusiana na watu waliomuunga mkono mke wake.