Kipindi cha Utamaduni na Sanaa kinakupeleka katika upishi na hususan uokaji mikate nchini Ujerumani. Mikate ikiwa ni chakula muhimu chenye kuchukua nafasi kubwa katika utamaduni wa vyakula vya kijerumani. Ni jambo la kawaida kuona maduka ya mikate kila kona ya mijini na hata vijijini. Ni kwa sababu kwa Wajerumani mikate ni chakula chao kikubwa cha kila siku, iwe asubuhi, mchana au jioni.