Vikosi vya Urusi vyashambulia kituo kikubwa cha kijeshi cha Ukraine karibu na mpaka na Poland. Viongozi wa Uturuki na Ugiriki kukutana leo juu ya vita ya Ukraine. Na kampuni ya gesi ya Urusi yasema itaendelea kusafirisha nishati hiyo kulingana na mkataba licha ya vita inayoendelea.