Kiongozi wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny amezuiliwa na polisi leo katika maandamano mjini Moscow siku mbili kabla kuapishwa kwa muhula wa nne kwa Vladimir Putin kama rais wa Urusi//Maelfu ya watu wameandamana leo katikati ya mji wa Paris Ufaransa wakipinga mabadiliko yaliyofanywa na Rais Emmanuel Macron mwaka mmoja baada ya kuingia madarakani.