1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashindano ya kuogelea yameahirishwa Paris kwa saa 24

1 Septemba 2024

Mashindano ya kuogelea katika michezo ya Olimpiki ya Walemavu,yaliyokuwa yamepangwa kufanyika leo Jumapili mjini Paris,yameahirishwa kwa kipindi cha saa 24 kufuatia kupunguwa kwa viwango vya ubora wa maji ya mto Seine.

https://p.dw.com/p/4k9LN
Michezo ya Olimpiki ya Walemavu huko Paris | Teresa Perales katika mbio za nyuma za mita 50 za wanawake
Michezo ya Olimpiki ya Walemavu huko Paris, Teresa Perales katika mbio za nyuma za mita 50 za wanawake. Picha: Sean M. Haffey/Getty Images

Mvua zilizonyesha siku mbili zilizopita katika mji huo mkuu wa Ufaransa zimesababisha mto huo kutokuwa na viwango vya kutumika, watu kuongelea.

Waandaaji wa mashindano hayo ya kuogelea pamoja na waandaaji wa michezo hiyo ya Olimpiki ya walemavu wamesema afya ya wanariadha ni suala linalopewa kipaumbele zaidi.

Mashindano yote 11 ya kuogelea yamepangwa kufanyika kesho Jumatatu, ikiwa ubora wa viwango vya maji ya mto huo utafikiwa.