1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Mashambulizi ya Urusi katika hospitali yaua watu saba

Saleh Mwanamilongo
28 Septemba 2024

Watu saba wameuawa kufuatia mashambulizi mawili ya Urusi, Jumamosi 28.09.2024, kwenye hospitali ya mji wa mpakani wa Sumy nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4lBv6
Ukraine yasema mashambulizi ya Urusi kwenye hospitali yaua watu saba
Ukraine yasema mashambulizi ya Urusi kwenye hospitali yaua watu sabaPicha: Sergei Gapon/National Police of Ukraine/AFP

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ukraine Igor Klymenko amesema bomu la kwanza lilimuuwa mtu mmoja na kuharibu sakafu kadhaa za hospitali na baada ya hapo, wagonjwa na wafanyakazi walianza kuhamishwa. Baadae shambulizi la pili lilifanyika na kuwauwa watu sita na kuwajeruhi vibaya wengine 12.

Ofisi ya polisi ya Ukraine imeyaita mashambulizi hayo mawili kuwa ya kijinga. Huku waendesha mashtaka wa Ukraine wakisema afisa mmoja wa polisi aliuwawa na mwingine kujeruhiwa. Duru za kiusalama za Ukraine zimesema mashambulizi hayo yalifanywa na droni za Urusi.

Mapema, Urusi ilisema vikosi vyake vinasonga mbele zaidi mashariki mwa Ukraine na kwamba vimechukua udhibiti wa kijiji cha Marynivka katika mkoa wa Donetsk, na sasa vinaelekea kwenye mji muhimu wa Pokrovsk.