Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas, anasema makubaliano ya nyuklia ya Iran hayana mbadala kwa sasa, baada ya waziri mwenzake wa Marekani Mike Pompeo kuyakosoa vikali makubaliano hayo ya mwaka 2015 na kutishia kuiadhibu vikali Iran, ikiwa haitobadili mwelekeo.