1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaMarekani

Maelfu ya watu wahamishwa Florida wakihofia kimbunga Helene

26 Septemba 2024

Maelfu ya wakaazi wa pwani ya Florida kusini-mashariki mwa Marekani, wameanza kuondoka kwenye makazi yao kutokana na hofu ya Kimbunga "Helene".

https://p.dw.com/p/4l5FR
Wakazi wa Florida wakiondoka kwa hofu ya kimbunga
Wakazi wa Florida wakiondoka kwa hofu ya kimbungaPicha: Joe Burbank/Orlando Sentinel/dpa/picture alliance

Kimbunga hicho kinatarajiwa kupiga leo Alhamisi, na kulingana na mamlaka kinaweza kuwa janga na kusababisha vifo.

Kituo cha utabiri wa matukio ya vimbunga nchini Marekani (NHC) kimesema kimbunga hicho kinatarajiwa kusababisha upepo mkali, mawimbi na mvua kubwa katika sehemu pana ya jimbo hilo. Gavana wa  Florida  Ron DeSantis ametangaza hali ya dharura kwa karibu kaunti zote 67 katika jimbo hilo.

Upepo kwa sasa umekadiriwa kufikia kasi ya kilomita 140 kwa saa na kimbunga hicho kinaweza kuipiga Florida leo jioni ​​baada ya kupiga eneo la kitalii la Yucatán huko Mexico. Majimbo kadhaa yaliyo jirani na Florida yako katika hali ya tahadhari ikiwa ni pamoja na jiji la Atlanta lenye wakazi milioni tano.