1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBrazil

Lula kuzungumza na Biden kuhusu uchaguzi wa Venezuela

Josephat Charo
30 Julai 2024

Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva na mwenzake wa Marekani Joe Biden watazungumza leo kwa njia ya simu kuhusu uchaguzi wa rais wa Venezuela wa Jumapili iliyopita uliosababisha machafuko.

https://p.dw.com/p/4ivJl
Rais Brazil Luiz Inacio Lula da Silva (kulia) na Guilherme Boulos
Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva, kulia, na Guilherme Boulos wa Chama cha Ujamaa na Uhuru, wakizindua uchaguzi wa Meya wa Boulos, huko São Paulo, Julai 20, 2024.Picha: Andre Penner/AP Photo/picture alliance

Kwa mujibu wa ikulu ya Marekani na serikali ya Brazil, mazungumzo hayo yalitarajiwa kufanyika mwendo wa saa nane na nusu saa za Marekani, lakini mada zitakazojadiliwa hasa, hazikutajwa. Kwa mujibu wa duru nchini Brazil, mazungumzo hayo ya simu yalipwangwa kufuatia ombi la serikali ya Marekani, huku ikijaribu kutafuta tathmini ya Brazilkuhusu matokeo ya uchaguzi katika taifa jirani yake la Venezuela.  Utawala wa Kremlin kupitia Dmitry Peskov, mkuu wa kitengo cha habari cha rais Vladimir Putin, leo umeutaka upinzani Venezuela ukubali matokeo. Mamlaka ya uchaguzi Venezuela ilimtangaza rais Nicolas Maduro mshindi kwa asilimia 51.2 ya kura.