1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUANDA: Ugonjwa unaofanana na Ebola wazidi kuuwa Angola.

4 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFQJ

Ugonjwa wa homa kali uliofanana na ugonjwa wa Ebola umewuwa watu 20 zaidi nchini Angola tangu siku ya alhamisi na kuongeza hesabu ya watu waliokwisha kufa kutokana na ugonjwa huo kufikia watu 146.

Shirika la afya duniani WHO limewapeleka watalaamu zaidi katika mkoa wa Uige kaskazini mwa mji mkuu wa Luanda kuongeza nguvu kazi na kuanzisha kituo maalum cha kukabiliana na visa vipya.

Ugonjwa huu wa kuambukiza hauna tiba na ni wachache wanaopata bahati ya kupona, unawashambulia zaidi watoto wa chini ya umri wa miaka 15.

Wanachi wa Angola katika mji mkuu wa Luanda wamo mbioni kununua madawa ya kusafishia nyumba ili kuepuka maambukizo.